Waziri wa afya: Atabatu Abbasiyya inafanya kazi kubwa ya kupambana na janga la Korona na tunatarajia kuona matunda yake katika mji wa Bagdad

Maoni katika picha
Waziri wa afya na mazingira Dokta Hassan Muhammad Tamimi amesifu kazi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na watumishi wake, wakiongozwa na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi katika kupambana na janga la Korona, ambazo wameanza tangu siku za kwanza yalipo gundulika maradhi hayo, akasema kuwa kazi hizo zinatokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye hiniza kushikamana dhidi ya janga hili na kusaidia taasisi za afya kwa ajili ya usalama wa wananchi na kuokoa watu walio ambukizwa, tunataraji kuona matunda ya kazi hizo katika mji wa Bagdad, kwa kujenga kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona chenye vitanda vingi.

Ameyasema hayo wakati anapokea ujumbe ulio ongozwa na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi, pamoja na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi Ustadh Jawadi Hasanawi na rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi Mhandisi Abbasi katika ofisi za wizara hiyo, alikuwepo pia Dokta Hazim Jamili mshauri wa waziri.

Makamo wa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumefanya ziara hii kwa ajili ya kumuonyesha waziri kazi zinazo fanywa na Ataba tukufu katika kipindi hiki kigumu, ikiwa ni pamoja na vituo ilivyo jenga kwa ajili ya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, ikiwa ni pamoja na wazo la ujenzi wa kituo kikubwa katika mji wa Bagdad, sambamba na kutengeneza vifaa vya kuwasaidia raia kujikinga na janga hili, kama vile barakoa, vitakasa mikono na kupuliza dawa ndani na nje ya mkoa wa Karbala”.

Akaongeza kuwa: “Tukamthibikitishia kuwa kazi zinazo fanywa na Ataba tukufu zinatokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, pia ni sehemu ya mradi wa kujenga vituo vya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona kwenye mikoa tofauti, aidha hatukusahau juhudi za madaktari wanaofanya kazi usiku na mchana katika kupambana na janga hili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: