(Maswabiihu..) sherehe za dua zilizo chaguliwa kutoka kwenye kitabu cha Swahifatus-sajadiyyah

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha fikra na ubunifu katika kitengo cha habari na utamaduni kimetoa kitabu cha (Maswabiih.. sherehe za dua zilizo chaguliwa kutoka kwenye kitabu cha Swahifatus-sajadiyyah) cha mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kitabu hicho kinajuzuu tatu, kinasherehe za dua zilizo chaguliwa kutoka kwenye kitabu cha Swahifatus-sajadiyyah ambazo ni (dua ya kumi na sita, dua ya kumi na saba, dua ya ishirini na dua ya thelathini na moja) kimechapishwa na Darul-Kafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Tumeongea na Ustadh Ridhwani Salami mkuu wa kituo hicho amesema kuwa: “Kituo kinakikosi maalum cha kazi hizi za kuhakiki na kuchapisha, tunamiradi mingi ambayo ipo katika utendaji, lakini kitabu hiki kina umaalum wake, mada zake zimetokana na sherehe za dua zilizopo kwenye kitabu cha Swahifatus-sajadiyya alizokuwa akitoa Mheshimiwa Sayyid kupitia khutuba za Ijumaa, kuanzia mwaka wa (2006) (2017) hadi mwaka huu”.

Akaongeza kuwa: “Kitabu hicho kimesajiliwa katika Darul-kutubi ya Iraq na kimewekwa namba ya utambulisho kimataifa ya (ISBN), hali kadhalika kimewekwa faharasi na kitengo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya na kitawekwa kwenye maonyesho ya vitabu ili kiingie mikononi mwa wasomaji”.

Akasisitiza kuwa: “Kikosi kazi kinaendelea kukamilisha kitabu cha sherehe ya dua ya Abu Hamza Shimali ambacho kimeandikwa na Mheshimiwa Sayyid Swafi pia”.

Akamaliza kwa kusema: “Mheshimiwa Sayyid amesifu kazi nzuri inayofanywa na kikosi kazi kwenye utangulizi wa kitabu, kitabu hicho kimewatia moyo zaidi, hususan pale aliposema: (Mwisho natoa shukrani za dhati kwa kila aliyesaidia kunakili khutuba hizi, kuzitoa kwenye maneno ya kusikika na kuziweka kwenye maandishi, pamoja na wale waliofanya kazi ya kusahihisha na kupangilia kitabu katika kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, Mwenyezi Mungu ailinde pamoja na Ataba zingine kwa jicho lake lisilolala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: