Idara ya kusafisha majengo ya vyoo inafanya kazi muda wote

Maoni katika picha
Idara ya kusafisha majengo ya vyoo chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kufanya kazi muda wote.

Bwana Riyadh Khadhwiir Hussein kiongozi wa idara ya kusafisha majengo ya vyoo amesema kuwa: “Idara yetu inawajibika kusafisha majengo ya vyoo katika mji mkongwe, watumishi wamegawanywa kwenye majengo yoe ya vyoo, ambayo jumla yapo (8) nane”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa majukumu ya idara hiyo ni kusafisha na kupuliza dawa muda wote saa (24), kazi ya kupuliza dawa na kudumisha usafi imeongezeka hivi karibuni kutokana na janga la Korona, wanatumia vifaa bora kutoka shirika la Khairul-Juud”.

Akasema: “Sehemu nyingu kuna upande wa wanaume na wanawake, pamoja na kuwepo sehemu za watu wenye mahitaji maalum kwenye kila jengo”.

Kumbuka kuwa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo vinavyo mhudumia zaairu moja kwa moja, nacho kinafanya kila kiwezalo kutoa huduma bora kwa mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: