Kituo cha kimataifa Al-Ameed kimechapisha toleo la (kumi na tisa na ishirini) la jarida la Albaahir-Ilmiyyah

Maoni katika picha
Kituo cha kimataifa Al-Ameed chini ya kitengo cha habari na utamaduni kaika Atabatu Abbasiyya tukufu kimechapisha toleo la (kumi na tisa na ishirini) la jarida la (Albaahir-Ilmiyyah) linalo andika taaluma ya mazingira na uhandisi, zimeandikwa tafiti tisa kwa lugha ya kiengereza.

Kuhusu swala hilo tumeongea na kamati mbili (kamati ya ushauri na wahariri) wamesema kuwa: “Toleo jipya -la kumi na tisa na ishirini- la jarida la Albaahir yameandaliwa na watumishi wa vituo hivyo baada ya kukubaliana umuhimu wa tafiti katika sekta tofauti, yote haya yanatokana na shauku ya kuendeleza utafiti hapa Iraq na duniani kwa ujumla, sambamba na kutumia fursa ya utafiti katika kugundua mambo mapya, na kufanyia kazi matokeo yote ya tafiti za kielimu”.

Akafafanua kuwa: “Kwakua jarida la Albaahir linaandika kuhusu mazingira na uhandisi, linatafiti nyingi kuhusu mambo hayo, hivyo ni jarida ambalo linatakiwa kuzingatiwa pamoja na kuandikwa katika wakati mgumu ambao taifa la Iraq linapitia kwa sasa”.

Akasema: “Tunaliweka mikononi mwa msomaji jarida la (Albaahir) ili kuchangia ukuwaji wa elimu kupitia tafiti na fikra za wataalam, pamoja na kuenzi tafiti zao, aidha kufanyia kazi matokeo ya elimu kwa maendeleo ya jamii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: