Mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kuandaa ramani ya kituo cha Alhayaat cha sita katika mkoa wa Muthanna

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, wanaofanya kazi kwenye mradi ya ujenzi wa kituo cha sita cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, kitakacho jengwa kwa ufadhili wa idara ya afya ya mkoa wa Muthanna chini ya hospitali ya Hussein (a.s), baada ya kukamilisha usanifu pamoja na wanufaika na kukamilika hatua ya kwanza ya maandalizi ya mradi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mhandisi Hasanaini Alaa Hussein mmoja wa wasimamizi wa mradi, akaongeza kuwa: “Kazi inaendelea kama ilivyo pangwa baada ya kumaliza maandalizi ya kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (3500), na kuchukua vipimo vyote tumeanza maandalizi ya hatua za kwanza za ujenzi”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya kumaliza kazi za awali tutaendelea na ujenzi wa tabaka la chini pamoja na vyoo halafu tutamwaga zege na ujenzi utaendelea katika hatua zingine”.

Akabainisha kuwa: “Kituo kitakua na vyumba (114) kama ilivyo kubaliwa na wanufaika sambamba na kuchukua tahadhari zote za kujilinda na maambukizi wakati wa ujenzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: