Maahadi ya Quráni itaanza harakati za majira ya kiangazi hivi karibuni kwa kutumia njia za mawasiliano ya kisasa

Maoni katika picha
Mkuu wa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya Shekh Jawadi Nasrawi amesema kuwa Maahadi itaanza harakati hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kufanya semina.

Nasrawi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Hivi karibuni Maahadi itaanza kufanya semina za Quráni na mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, zikiwemo semina za maarifa ya Quráni, kuhifadhi na kusoma Quráni tukufu, mambo yote yatafanywa kwa njia ya mtandao, tutawafikia wanafunzi wakiwa majumbani kwao, ili kuwaendeleza katika masomo ya Quráni kwa njia salama na kwa kufuata maelekezo ya taasisi za afya.

Akaongeza kuwa: “Maamuzi haya yamefikiwa baada ya kufanya vikao vingi pamoja na vituo na matawi ya Maahadi kwa njia ya mtandao, ambapo tumejadili njia bora ya kuendelea kufundisha masomo ya Quráni katika mazingira haya ya maambukizi ya virusi vya Korona, vinavyo sababisha harakati nyingi kusimama, aidha tukajadili umuhimu wa miradi ya Quráni kiimani, tukakubaliana kutumia njia za mawasiliano ya mitandao ya kisasa kuwafikia wanafunzi wetu na kuwafundisha kilicho pangwa kufundishwa”.

Akasisitiza kuwa: “Njia za ufundishaji na ratiba za masomo zitazingatia umri wa mwanafunzi na kiwango cha elimu yake na ulazima wa masomo anayotakiwa kufaulu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: