Kumaliza sehemu ya pili katika ujenzi wa kituo cha Alhayaat katika mkoani Muthanna na kuanza ujenzi wa boma la chuma

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wameanza kujenga boma la chuma katika kituo cha Alhayaat cha sita cha kutibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mkoa wa Muthanna, baada ya kumaliza sehemu ya pili ya mradi huo.

Mhandisi msimamiaji wa mradi bwana Swafaa Muhammad Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi zinaendelea kama zilivyo pangwa, mafundi wanajitahidi wamalize mradi ndani ya muda uliopangwa na kwa viwango vinavyo takiwa”.

Akaongeza kuwa: “Tumemaliza sehemu ya pili na sasa tumeingia sehemu ya tatu ya (BRC)”.

Akasema: “Tumeanza kujenga boma la chuma pamoja na ujenzi wa chini unaohusisha njia za maji taka na mfumo wa maji na mengineyo”.

Akafafanua kuwa: “Mafundi wanafanya kazi kwa ari kubwa hadi usiku”.

Kumbuka kuwa mradi huu inajengwa kwa ufadhili wa idara ya afya ya Muthanna chini ya hospitali ya Hussein (a.s), kwa maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi yanayo tokana na muongozo wa Marjaa Dini mkuu unaohimiza kusaidia sekta ya afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: