Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wameanza kupuliza dawa katika mji wa Baabil

Maoni katika picha
Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha waliganaji (Liwaau/26 Hashdu Shaábi) katika mkoa wa Baabil, wameanza kupuliza dawa kwenye majengo ya serikali ya mkoa huo.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: “Tumepuliza dawa kwenye ofisi za serikali pamoja na maeneo ya katikati ya mji, tumepuliza kwenye vitengo vyote na kumbi za kutolea huduma kwa wananchi hadi katika njia za kuelekea kwenye maeneo yanayotoa huduma za kijamii”, akasema kuwa kazi bado inaendelea hadi tufikie vitongoji vyote na mitaa ya mkoa wa Baabil.

Tambua kuwa kikosi cha Abbasi kiliunda kamati maalum ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona yenye jukumu la kupuliza dawa kwenye maeneo yote ya makazi ya watu, ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: