Kumbukumbu ya kifo cha Imamu Swadiq (a.s): wingu la huzuni limetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Macho yanalia na kububujika machozi * yanamhuzunikia aliyezikwa Baqii.

Macho yanalia damu kwa kumkosa kiongozi * katika Aali Muhammad hakuna wa mfano wake.

Macho gani yasiyo toka machozi * kwa kuhuzunikia kifo cha Jafari bun Muhammad.

Huzuni imetanda katika Atabatu Abbasiyya na kuta zake zimewekwa mapambo meusi kwa ajili ya kuomboleza kifo cha mwezi wa sita miongoni mwa miezi ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), Imamu Abu Abdillahi Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s), na kuwapa pole watu wa nyumba ya Mtume (a.s) ikiwa ni sehemu ya kufanyia kazi kauli ya anaye ombolezwa kifo chake isemayo (Huisheni mambo yetu Mwenyezi Mungu amrehemu atakaye huisha mambo yetu).

Bendera za kuomboleza zimepandishwa na mabango yaliyo andikwa maneno ya kuomboleza yamewekwa ndani ya haram tukufu kutokana na msiba huu mkubwa kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (s.a).

Atabatu Abbasiyya tukufu kama kawaida yake kwenye kila tukio la msiba huandaa ratiba maalum, kutokana na mazingira ya maambukizi ya virusi vya Korona pamoja na maelekezo ya idara ya afya, kutakuwa na muhadhara utakao ruswa mubashara na mitandao ya mawasiliano ya jamii utakao tolewa na mmoja wa mashekh wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, ukiwemo mtandao wa kimataifa Alkafeel na mingine, mhadhiri atakuwa ni Sayyid Muhammad Mussawi atazungumza kwa vikao kumi, ataongelea historia ya Imamu huyo (a.s), pamoja na kaswida za kuomboleza zitakazokuwa zinawekwa na kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: