Watumishi wa kikosi cha Abbasi wanapuliza dawa katika mkoa wa Basra

Maoni katika picha
Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu Shaábi) katika mkoa wa Basra wanapuliza dawa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: Katika opresheni hiyo wameshiriki watu wengi wakujitolea, wameanzia sehemu ya Khaura hadi Baladiyya, akasema kuwa kazi itaendelea kazika maeneo mengi ya mkowa huo siku zijazo.

Shughuli hii ni muendelezo wa shughuli nyingi zinazo fanywa na kikosi cha Abbasi (a.s) kupitia wawakilishi wake kwenye mikoa tofauti ya Iraq kwa kutumia vifaa vya kisasa vwenye uwezo mkubwa wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Tambuwa kuwa kikosi cha Abbasi kiliunda kamati maalum kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona na kimefanya kazi ya kupuliza dawa kwa ajii ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo katika maeneo ya makazi ndani na nje ya mji mtakatifu wa Karbala, na inafanya kila iwezalo katika kutekeleza swala hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: