Maktaba ya wanawake imepata mwitikio mkubwa wa kongamano la kimataifa lililofanywa kwa njia ya mtandao katika chuo kikuu cha Dhiqaar

Maoni katika picha
Maktaba ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki kwenye kongamano la kimataifa lililofanywa kwa njia ya mtandao kwa mara ya kwanza chini ya usimamizi wa kitivo cha habari katika chuo kikuu cha Dhiqaar lenye anuani isemayo: (Khutuba za kielimu na utamaduni mbadala) kupitia jukwaa la (ZOOM MEETING) siku ya Jumatano mwezi (24 Shawwal 1441h) sawa na (17 Juni 2020m) lililokuwa na ushiriki wa kitaifa na kimataifa ambao ni watalam na wabobezi wa mambo mbalimbali.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na kiongozi wa maktaba ya wanawake bibi Asmaa Abedi amesema kuwa: “Kongamano hilo limetokana na ushirikiano wa maktaba ya wanawake unaolenga kuendeleza mawasiliano katika wakati huu wa janga la Korona, miongoni mwa vipaombele vyake ni kudumisha mawasiliano kwa kutumia mitandao ya mawasiliano ambayo inawezesha mawasiliano hayo kwa njia tofauti, maktaba imepiga hatua kubwa katika swala hilo, ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya makongamano ya kielimu na kitafiti”.

Akaongeza kuwa: “Ushiriki wetu kwenye kongamano hili ulikuwa kwa ajili ya kutoa mada ya kitafiti, tulizungumza mada yetu kwenye kikao cha kwanza, mada ilikuwa inasema: (Wanahabari wa kike wanaunda jamii bora.. Jarida la Riyadhu Zahraa kama mfano), tuliangazia changamoto ambazo jarida linajaribu kuzitatua, sambamba na kuangalia umuhimu wa jarida la wanawake katika kuhamasisha jamii ya wanawake wa Iraq, linasaidia kujenga uwelewa katika mambo ya kitamaduni, kijamii na kisiasa, mambo hayo yana athari kubwa katika jamii ambayo mwanamke ni kiumbe muhimu”.

Kumbuka kuwa kongamano limepata washiriki wengi kutoka ndani na nje ya Iraq, wamebadilishana uzowefu mbalimbali kuhusu utamaduni na vyombo vya habari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: