Kwa kutumia kifaa tiba cha (Faco) mzee wa miaka sabini amerudisha uwezo wa kuona katika hoapitali ya rufaa Alkafeel

Maoni katika picha
Timu ya upasuaji wa macho katika hospitali ya rufaa Alkafeel, imetangaza kufanikiwa kurudisha uoni wa bibi mwenye miaka zaidi ya sabini uliokua umepotea kwa sababu ya macho yake kujaa maji meupe.

Dokta Salami Karáwi amesema kuwa: “Timu ya upasuaji chini ya usimamizi wetu imefanikiwa kumtibu bibi mwenye umri wa miaka (74) aliyekuwa na tatizo la maji meupe kwenye jicho lake la kulia lililosababisha kupoteza uwezo wa kuona”.

Akabainisha kuwa: “Matibabu hayo yamefanywa kwa kutoa maji meupe kwenye jicho lake kwa kutumia kifaa cha (Faco) kinacho julikana kama kifaa cha kukamulia chicho, matibabu ya kutoa maji kwenye jicho na kuweka mengine kwa njia salama”.

Tambua kuwa: “Teknolojia hiyo inahitaji upasuaji mdogo tofauti na ule uliozoweleka, pia muda wa matibabu hayo ni mfupi ukilinganisha na muda wa matibabu yaliyo zoweleka, na humaliza tatizo lote, jicho hurudisha uwezo wa kuona vizuri, kwa kuwa kuna kifaa huwekwa ndani ya jicho huwa ni salama zaidi tofauti na miwani”.

Akaongeza kuwa: “Mgojwa amerudi nyumbani baada ya saa moja tangu alipo fanyiwa matibabu, ameendelea na kazi zake kama kawaida akiwa na hali nzuri”.

Fahamu kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma bora daima kwa kutumia teknolojia na vifaa tiba vya kisasa pamoja na umahiri wa madaktari wake wenyeji na wageni hapa nchini, jambo ambalo limeifanya itoe ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa maradhi tofauti, pamoja na kupokea wagonjwa ambao wapo katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: