Watumishi wa kikosi cha Abbasi wanaendelea kupuliza dawa katika mji wa Diwaniyya

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) wanaendelea kupuliza dawa ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona katika mkoa wa Diwaniyya, wamepuliza dawa kwenye mitaa kadhaa na taasisi za serikali.

Msemaji wa kikosi ameriboti kuwa: sehemu zilizo pulizwa dawa ni duka la kubadilisha pesa la Twiful-Islami, ofisi ya Muruur Diwaniyya na eneo la Twawarii ya pili.

Akaongeza kuwa: kisha wakaenda kupuliza dawa kituo kinacho unganisha barabara ya (Bagdad – Shumili – Dagharah).

Akasisitiza kuwa kazi ya kupuliza dawa itaendelea hadi tatizo la virusi vya Korona litakapo isha.

Akasema kuwa kazi ya upulizaji wa dawa inafanywa kwa kutumia vifaa vya kisasa.

Tambua kuwa iliundwa kamati maalum ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona yenye jukumu la kupuliza dawa katika makazi ya watu ndani na nje ya mkoa wa Karbala, inafanya kila iwezalo katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: