Maahadi ya Quráni tawi la Hindiyya inaendelea kutoa elimu kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Wanafunzi wa idara ya tahfiidh chini ya Maahadi ya Quráni/tawi la Hindiyya, inaendelea kutoa elimu kwa njia ya mtandao ili kukamilisha ratiba ya kuhifadhisha kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu, na kudurusu sehemu walizo hifadhi.

Wameendelea kufundisha kwa njia ya masafa na kufuata kanuni zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, masomo hayo ni muhimu kwa kuwajenga wanafunzi na kuendeleza huduma za Maahadi kwa vizito viwili.

Tambua kuwa masomo hayo ni moja ya semina nyingi zinazo endeshwa na Maahadi kwa njia ya mtandao kwenye mikoa tofauti, na kuendelea kuitumikia Quráni pamoja na kuwepo kwa balaa la maambukizi ya virusi vya Korona.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, hutoa mafunzo mbalimbali ya Quráni kila mwaka, lakini kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa sambamba na tahadhari za kujikinga na maambukizi zinazo fanywa na Ataba tukufu, tumetosheka na kufanya mambo machache kwa njia ya mtandao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: