Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wanakaribia kumaliza hatua ya kwanza ya ukarabati wa baadhi za sehemu katika hospitali ya Karbala ya watoto

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wanafanya kazi ya kukarabati baadhi ya maeneo katika hospitali ya Karbala ya watoto, wanakaribia kumaliza hatua ya kwanza.

Tumeongea na Mhandisi Muhammad Twawil kuhusu maendeleo ya kazi hiyo, amesema kuwa: “Kazi inaendelea vizuri katika hospitali ya Karbala ya watoto, tunakarabati sehemu zote za vyoo katika hospitali hiyo, pamoja na kuweka marumaru baadhi za sehemu na kupaka rangi”.

Akaongeza kuwa: “Tupo karibu ya kumaliza hatua ya kwanza, inayo husisha ukarabali wa sehemu tatu za vyoo, tumekamilisha kazi kwa asilimia %75”.

Akafafanua kuwa: “Tumegawa kazi katika hatua nne kulingana na ratiba, ugawaji huo utasaidia kufikia kila sehemu ya hospitali, pamoja na kufanya matengenezo mengine kama vile kuweka marumaru na kupaka rangi kwenye kuta, kazi zote zinafanywa kwa kufuata vigezo na wasifu unaotakiwa na uongozi wa hospitali”.

Tambua kuwa Kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kina kazi kubwa ya ujenzi na ukarabati vituo vya ndani na nje ya Ataba, chini ya mafundi mahiri wenye uzowefu mkubwa wa kazi za ujenzi, hivi karibuni wamekuwa wakifanya ujenzi wa vituo vya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: