Kuanza hatua ya nne kwenye sehemu ya kwanza ya ujenzi wa mradi wa kituo cha Alhayaat katika mji wa Bagdad

Maoni katika picha
Mapema leo asubuhi mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wameingia hatua ya nne ya ujenzi wa sehemu ya kwanza katika mradi wa kituo cha Alhayaat cha tano cha kutoa huduma kwa watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji mkuu wa Bagdad, kinacho jengwa katika hospitali ya Ibun Qafu upande wa Raswafa, hatua hiyo imehusisha kukata vyumba kwa kutumia (Sandwich panel) katika boma la chuma lililokamilika hivi karibuni.

Kwa mujibu wa maelezo ya mmoja wa wahandisi wakazi Ali Hiru, amesema kuwa: “Hatua ya nne ni miongoni mwa sehemu muhimu katika ujenzi huu wenye ukubwa wa mita za mraba (1377) vyumba (56) kutoka jumla ya vymba (118) vitakavyo jengwa, tumevigawa sehemu tatu, hatua hii itakuwa na kazi zifuatazo:

  • - Kuchukua vipimo vya lazima vya sehemu zote ikiwa ni pamoja na vyumba.
  • - Kukata vyumba kwa kutumia (sandwich panel) kwa kufuata vipimo maalum.
  • - Kuweka vitenganishi katika boma la chuma.
  • - Kuweka madirisha na milango inayo tengenezwa hivi sasa katika kitengo cha usimamizi wa kihandisi.
  • - Kiweka (PVC) kwenye vyoo vyote vya vyumbani pamoja na kufanya maandalizi ya kuweka sakafu”.

Akasisitiza kuwa: “Kazi hizi ni sehemu ya kuandaa kazi za hatua inayo fuata, nayo ni hatua ya kuweka Jipsam bord pamoja na kazi zingine za kumalizia ujenzi huo, na kuhakikisha shughuli zote zinaendelea kama zilivyo pangwa bila kusimama, mafundi wetu wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanamaliza kazi ndani ya muda uliopangwa”.

Tambua kuwa ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha tano unafanywa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (5000) jengo litakuwa na vyumba vya wagonjwa (118) pamoja na vyumba vingine vya idara na utumishi, kituo hiki ni moja ya vituo vitatu ambayo vinajengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katuka Atabatu Abbasiyya tukufu, kwenye mkoa wa Bagdad, Muthanna na Karbala, pia ni sehemu ya kukamilisha vituo vitatu vya awali, cha kwanza katika mji wa Hussein (a.s) wa kitabibu, cha pili katika hospitali kuu ya Hindiyya na kituo cha tatu kilijengwa chini ya ufadhili wa hoapitali ya Amiirulmu-Uminiin (a.s) katika mkoa wa Najafu Ashraf.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: