Mradi wa ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha tano katika mji wa Bagdad umekamilika kwa zaidi ya asilimia %30 na ujenzi unaendelea

Maoni katika picha
Mafundi wanaojenga kituo cha Alhayaat cha tano kwa ajili ya kutibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona, mradi unaotekelezwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kusaidia idara ya afya ya mkoa wa Bagdad, wamesema kuwa sehemu ya kwanza imekamilika kwa zaidi ya asilimia %30, na ujenzi unaendelea, wanafanya kazi zaidi ya saa (18) kwa siku, ujenzi huu unatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi ujao au mwanzoni mwa mwezi wa nane.

Mhandisi Ali Hiru mmoja wa wahandisi wakazi wa mradi huo amesema kuwa: “Uwanja unaojengwa kituo hiki unaukubwa wa mita za mraba (5000) tumegawa kazi sehemu tatu kwa ajili ya kuzuwia muingiliano wa kazi, (ufungaji wa sandwich panel kwenye boma la chuma katika hatua ya kwanza inayo husisha eneo la mita za mraba (1377) yenye vyumba (56) umekamilika kwa zaidi ya asilimia %50”.

Akaongeza kuwa: “Kazi zingine za hatua hiyo zimekamilika kwa asilimia %100 huku sehemu zingine zikiendelea hatua baada ya hatua, na kiwango cha ukamilifu wake ni kizuri”.

Akabainisha kuwa: “Sehemu ya pili tuliyo maliza kuweka msingi yenye ukubwa wa mita za mraba (1377) yenye vyumba (56) kazi ya kukata vyumba kwenye boma la chuma imesha anza nayo ni sehemu ya maandalizi ya kuingia hatua ya tatu”.

Kumbuka kuwa kituo cha Alhayaat cha tato ni sehemu ya vituo vitatu vinavyo jengwa na mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, kwenye mkoa wa Bagdad, Muthanna na Karbala, aidha ni sehemu ya muendelezo wa kituo kilicho jengwa katika mji wa Hussein (a.s) wa kitabibu na katika hospitali ya Hindiyya mkoani Karbala, huku kituo cha tatu kikijengwa kwa ufadhili wa hospitali ya Amirulmu-uminina (a.s) katika mkoa wa Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: