Harakati mbalimbali zinaendelea katika chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya kipo katika maandalizi ya kuwapa mitihani wanafunzi wake waliosoma kwa njia ya mtandao.

Miongoni mwa warsha zilizo fanywa na idara ya taaluma ni warsha ya (namna ya kufanya mitihani kwa kutumia program ya UIMS) ambayo ni program maalum ya chuo kikuu cha Alkafeel, kwa kushirikiana na kitengo cha utalii wa kidini chini ya usimamizi wa idara ya teknolojia na taaluma, wahadhiri wa warsha hiyo walikuwa ni mkufunsi wa aina za ubinaadamu, mkufunzi wa kitivo cha sheria na vigawanyo vyake na mkufunzi wa habari na utalii wa kidini.

Aidha warsha hiyo imejikita katika kufafanua namna ya kutuma maswali kwa njia ya mtandao na namna sahihi ya kutumia program hiyo, pia kulikuwa na maswali na maoni mbalimbali kutoka kwa washiriki, wahadhiri walijibu na kutoa ufafanuzi zaidi.

Mwisho; wahadhiri wametoa shukrani nyingi kwa uongozi wa chuo kwa kuwapa fursa ya kutambua program hiyo.

Tambua kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kimesha fanya warsha nyingi za walimu na wanafunzi, kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi wake wanafanya mitihani kama kawaida.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: