Mitambo ya Oksijen ni tegemeo kubwa katika hospitali ya Hussein

Maoni katika picha
Mhandisi mtendaji katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ali Razaaq, amesema kuwa mitambo ya Oksijen iliyo fungwa na Ataba tukufu katika hospitali ya Hussein na Dhiqaar inaumuhimu mkubwa.

Akaongeza kuwa: “Mitambo hiyo inatumia mfumo wa (psa) kusambaza Oksijen kwenye mitungi ya gesi, na kuondoa aina zote za gesi na kubakiza Oksijen pekeyake”.

Akafafanua kuwa: “Mitambo hiyo inafanya kazi saa (24) kwa kiwango cha mita (36) kwa saa, mitambo hiyo ni tegemeo kubwa la Oksijen na inasaidia kupambana na tatizo la ukosefu wa bidhaa hiyo muhimu katika kutibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya asubuhi ya Jumatano mwezi (9 Dhulqaada 1441h) sawa na tarehe (1 Julai 2020m) ilianza kazi ya kufunga mitambo ya Oksijen katika hospitali ya Hussein mkoani Dhiqaar, chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi kufuatia maombi ya idara ya hospitali hiyo kwa Ataba tukufu, ya kupatiwa gesi ya Oksijen na kuokoa wagonjwa wa Korona walio lazwa kwenye hospitali hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: