Kwa ushiriki wa zaidi ya wataalam wa maktaba 600: maktaba ya wanawake inashiriki kwenye kungamano la kimataifa nchini Baharain

Maoni katika picha
Maktaba ya wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya imeshiriki kwenye kongamano la kimataifa linalo simamiwa na jumuiya za maktaba za Baharain chini ya anuani isemayo: (Nafasi ya maktaba na vituo vya elimu katika mazingira ya janga la Korona), kongamano hilo linazaidi ya washiriki (600) kutoka nchi ishirini za kiarabu na zisizokua za kiarabu, linaendeshwa kwa kutumia program ya (zoom cloud meetings).

Tumeongea na kiongozi wa maktaba ya wanawake bibi Asmaa Raád amesema kuwa: “Ushiriki wa kongamano hili ni sehemu ya ratiba ya kushiriki kwenye makongamano, nadwa na warsha zinazo fanywa katika kipindi hiki cha janga la virusi vya Korona, maktaba imewakilishwa na bibi Lamyaa Hussein Mahmood kutoka idara ya kusaidia usomaji”.

Akaongeza kuwa: “Kongamano hilo limeangazia mikakati ya kiutendaji inayo fanywa na maktaba za wanawake, pamoja na program inayo tumika kuwahudumia wanufaika, kama vile program ya kutoa huduma kwa mbali (masafa) inayo tumiwa na maktaba pamoja na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Bibi Asmaa akasisitiza kuwa: “Washiri wa kongamano wamepongeza maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu na wakasema kuwa imekuwa ya kwanza daima katika kuleta vitu bora”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: