Toleo la saba la jarida kuhusu turathi za Karbala

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimechapisha matoleo mawili ya jarida la saba miongoni mwa majarida ya (turathi za Karbala) toleo la mwaka (2020m) ambalo limeandaka kwa undani kuhusu turathi za Karbala.

Chapisho hili ni la ishirini na tatu na ishirini na nne katika jarida la turathi za Karbala, kiidadi ni la kwanza na la pili katika jarida la saba, ndio toleo kubwa katika mwaka wa saba wa umri wa jarida hili, limesheheni zaidi ya mada mia mbili na ishirini kuhusu turathi mbalimbali.

Miongoni mwa mada hizo zipo zinazo angazia mafunzo kutoka kwa bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) katika turathi za Karbala, pamoja na mada kuhusu tarjama, Rijali, Usuul, Faharasi, Adabu, Historia na masomo ya hadithi, aidha kimefanyiwa uhakiki kitabu cha (Majaalisul-Mawaaidh) cha shekh Muhammad Taqi bun Hussein Ali Harwi Alhaairiy cha mwaka (1217/1299h).

Kwa ajili ya kukamilisha kazi iliyo fanywa na kamati ya wahariri wa jarida, ya kuhakiki aina mbalimbali za turathi, jarida linasisitiza kuwa milango yake iko wazi kwa kila muandishi, na linatoa wito kwa waandishi wajitokeze kuandika tafiti mbalimbali, kuna mambo mengi ambayo tunatakiwa kuyazingatia, ikiwa ni pamoja na matukio ya kihistoria na kisiasa katika mji wa Karbala, hususan matukio ambayo hayajawahi kuandikwa, sambamba na masomo mengine ya kiislamu, kama vile Quráni, Fiqhi na Usuul, Hadithi pamoja na kuhakiki nakalakale za wanachuoni wa Karbala.

Ili kupakua jarida jarida (vitabu) hivyo tumia link zifuatayo:

  • 1- https://karbalaheritage.alkafeel.net/index.ph p?res=55
  • 2- https://www.iasj.net/iasj?func=issueTOC&isId=11158&uiLanguage=ar
    Kushiriki katika kutuma tafiti tumia barua pepe ifuatayo:

turath@alkafeel.net

au toghuti ya jarida:

http://karbalaheritage.alkafeel.net/

au parua pepe ya rais wa wahariri.

drehsanalguraifi@gmail.com

au peleka moja kwa moja kwenye ofisi za jarida zifuatazo:

(Iraq/ Karbala tukufu/ mtaa wa Baladiyya/ tawi lililopo mkabala na jengo la hoteli ya Baitul-Juud/ karibu na taasisi ya Maasumina kumi na nne).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: