Baada ya mkoa wa Karbala, Najafu, Bagdad na Muthanna: Atabatu Abbasiyya inaitikia wito wa Baabil, na imeanza kujenga kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeitikia wito wa watu wa Baabil, imeanza kujenga kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona Alhayaat cha saba, ambacho ni muendelezo wa vituo vilivyo jengwa katika mkoa wa Karbala, Najafu, Bagdad na Muthanna.

Kwa mujibu wa maelezo ya makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussa.

Amesema: “Baada ya kupokea maombi kutoka kwa idara ya afya ya mkoa wa Baabil ya kujenga kutuo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona Alhayaat, na kufuatia uwezo wa kuhudumia wagonjwa hao, ikiwa ni sehemu muhimu ya kusaidia sekta ya afya katika mkoa huu, tumefanya haraka kuitikia wito wao pamoja na kuwa mafundi wetu wanaendelea na kazi kama hiyo katika mkoa wa Karbala, Bagdad na Muthanna”.

Akabainisha kuwa: “Kituo kitajengwa katika mji wa Marjani wa kitabibu kwa kuwashirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Baabil, kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (3500), kitakuwa na zaidi ya vyumba (85) pamoja na vyumba vya madaktari na wauguzi, kwa mujibu wa makadirio ya awali, tayali mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wamesha anza kuandaa sehemu kitakapo jengwa kituo hicho, na wanaendelea na kuandaa ramani maalum ya ujenzi huo, wataanza kujenga baada ya makubaliano ya mwisho na upande wa wanufaika, ili kuhakikisha wanatoa huduma bora za matibabu kwa watu wa Baabil”.

Kumbuka kuwa jengo hili ni moja ya vituo vitatu vinavyo jengwa na mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kwenye mkoa wa Bagdad, Muthanna na Karbala, aidha ni sehemu ya muendelezo wa vituo vingine vitatu vilivyo jengwa, katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu, kingine katika hospitali kuu ya Hindiyya na cha tatu kilijengwa kwa ufadhili wa kiongozi wa waumini (a.s) katika mkoa wa Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: