Atabatu Abbasiyya imekabidhi zawadi kwa viongozi wa mafundi na wahandisi wake

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya imekabidhi zawadi kwa viongozi wa mafundi na wahandisi wake katika mkoa wa Karbala, kama sehemu ya kupongeza kazi za ujenzi wanazofanya na kupendezesha mji huu mtakatifu.

Hafla ya kukabidhi zawadi imefanywa ndani ya ukumbi wa mgahawa wa Atabatu Abbasiyya na kuhudhuriwa na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar na jopo la wajumbe wa kamati kuu pamoja na rais wa kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili takatifu.

Katibu mkuu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Atabatu Abbasiyya imekuwa mstari wa mbele mara zote katika kuonyesha shukrani kwa kazi yeyote inayofanywa kwenye mkoa huu, leo baada ya kushuhudiwa maendeleo ya miradi ya ujenzi tumeamua kutoa zawadi kwa mafundi na wahandisi kutokana na kazi nzuri wanayo fanya, tuna amini kuwa zawadi zinawapa moyo na kuwashajihisha zaidi, ukizingatia kuwa mkoa huu unastahiki maboresho zaidi kutokana na utukufu wake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: