Katika kuhuisha turathi za fikra ya Husseiniyya: kituo cha turathi za Karbala kimetoa kitabu cha (Siku ya Twafu) chenye vipengele vitano

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimetoa chapisho la kitabu cha (Siku ya Twafu.. kuuwawa kwa Imamu Abu Abdillahi Hussein Shahid –a.s-), kutokana na uandishi wa Ayatullah Ustadh Shekh Haadi Najafiy, kimerejewa na kuwekwa faharasi na wataalamu wa kituo tajwa.

Kitabu kinakurasa (343), kimeandika kuhusu siku ya Twafu na yaliyo jiri, kimekusanya kisa cha Imamu Abu Abdillahi Hussein bwana wa mashahidi (a.s), na mambo yote yaliyo tokea siku ya Ashura mwaka wa stini na moja hijiriyya na yaliyo fuatia.

Kitabu kinasehemu tano zifuatazo:

  • - Sehemu ya kwanza vita dhidi ya Imamu Hussein (a.s) na maandalizi yake.
  • - Sehemu ya pili mashahidi katika wafuasi waka (r.a).
  • - Sehemu ya tatu mashahidi katika kizazi cha Abu Twalib (a.s).
  • - Sehemu ya nne kuuwawa kwa Imamu Abu Abdillahi Hussein (a.s).
  • - Sehemu ya tano yaliyo tokea baada ya kuuwawa kwa Imamu (a.s).
  • - Mwisho yameandikwa yaliyo tokea Twafu miongoni mwa habari za pande mbili.

Tambua kuwa msomaji anaweza kupata kitabu hicho pamoja na machapisho yote na harakati zinazo fanywa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu pamoja na taarifa za kituo hiki kupitia toghuti ifuatayo www.mk.iq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: