Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya anasaidia harakati za ustawi wa jamii dhidi ya janga la Korona

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya ambae ndio mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) Maitham Zaidi, ameahidi kuzipa vitu wanavyo hitaji idara ya ustawi wa jamii kwa ajili ya kupambana na janga la Korona.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa makao mkuu ya kikosi wamefanya kikao na idara za ustawi wa jimii zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya huko mikoani kwa usimamizi wa Zaidi, wakajadili kuhusu namna ya kuendelea na kupambana na janga la Korona kutokana na nafasi kubwa ya idara hizo kwenye vita hiyo, hasa katika maeneo ambayo yameripoti visa vya maambukizi.

Naye kiongozi wa idara ya ustawi wa jamii bwana Qassim Maámuri akasema kuwa: “Kikao kimejadili mahitaji muhimu katika swala hilo, hasa vifaa kinga (barakoa na dawa za kupuliza), makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya kiongozi wa kikosi cha Abbasi ameahidi kusaidia vifaa hivyo kwa kiwango wanacho hitaji ili kuvuka salama kwenye kipindi hiki”.

Sayyid Baadi Zaamiliy kiongozi wa idara ya ustawi wa jamii katika mkoa wa Waasit amesema kuwa: “Hakika kikao kimekuwa na matunda mazuri, maombi yetu yamekubaliwa, tumejadili kuhusu harakati za kibinaadamu, kama vile kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo, familia za mashahidi na wahanga wa janga la Korona”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: