Rais wa chuo kikuu cha Alkafeel amesema kuwa: Program ya Siraaj inayotumiwa na vyuo vikuu inakusanya baina ya uzowefu wa vyuo vikuu vya kimataifa na mazingira ya kielimu ya Iraq

Maoni katika picha
Program ya Siraaj iliyo tengenezwa na kituo cha taaluma Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya chuo kikuu cha Alkafeel, na sasa inatumiwa na vyuo vikuu vingine pia, imekubalika sana kwenye uwanja wa elimu na katika wizara ya habari.

Rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dkt Nuuris Dahaani amesema kuwa: “Chuo kikuu cha Alkafeel kimetengeneza mazingira mazuri ya elimu kwa wanafunzi wake, ndio desturi ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa taasisi zake zote huhakikisha zinatoa huduma bora”.

Akaongeza kuwa: “Program ya Siraaj ni tunda lililotokana na juhudi za chuo katika kuhakikisha kinaendana na maendeleo ya kielimu na teknolojia sawa na vyuo vikuu vingine vya kimataifa, kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika ufundishaji”.

Akasisitiza kuwa: “Kazi hii imeonyesha utaalamu mkubwa wa teknolojia uliopo katika kituo cha taaluma Alkafeel, kilicho tengeneza program hii kwa kufuata maelekezo ya viongozi wa chuo, na mazingira ya elimu ya Iraq pamoja na muongozo wa wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu”.

Tambua kuwa msimamizi wa idara ya ufundishaji kwa njia ya mtandao katika wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu Dokta Aamir Salim Amiir, amesema kuwa Program ya Siraaj imekamilisha vigezo vya ufundishaji vya Iraq.

Kumbuka kuwa Program ya Siraaj inayo tumiwa na vyuo vikuu ilitengenezwa na kituo cha taaluma Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kama sehemu ya kukidhi mahitaji ya vyuo, ya kuwepo kwa program ya kimtandao.

Kwa maelezo zaidi piga siku kwa namba zifuatazo: 07602323004 / 07711711190.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: