Idara ya masomo na utafiti wa Quráni inaendelea kufanikisha mkakati wake wa kielimu

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea na harakati zake za kueneza utamaduni wa kufuata mafundisho ya Quráni, kupitia matawi yake yote yaliyopo mikoani hapa nchini, idara ya masomo na utafiti wa Quráni katika Maahadi ya Quráni tawi la Najafu inaendeleza harakati zake maarufu za Quráni.

Miongoni mwa harakati hizo ni kuandika machapisho kuhusu Quráni, miongoni mwa machapisho hayo ni (vitavu, tafiti fupifupi na Makala), sambamba na kuboresha selebasi za masomo, hususan katika sekta ya kuhifadhi Quráni na usomaji wake pamoja na kuhakiki nakala-kale za Quráni, hasa zinazo husu elimu ya tajwidi.

Idara inaendelea kuandaa faharasi na kufanya tafiti za vitabu vya masomo ya Quráni tukufu, hususan uandishi wa sasa.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya imezowea kufanya harakati mbalimbali kuhusu Quráni kila mwaka, lakini kutokana na hali ya mwaka huu na tahadhari inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona itatosheka na harakati chate.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: