Mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamemaliza kuandaa mchoro wa ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha saba katika mji wa Baabil

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamemaliza kuandaa mchoro wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona cha saba katika mkoa wa Baabil, na wameanza kazi za awali za kujenga msingi.

Mhandisi mkazi wa mradi Ammaar Swalahu Mahadi amesema kuwa: “Mradu unajengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuusaidia mkoa wa Baabil kupambana na janga la Korona, kwenye uwanja wenye ukubwa wa mita (3500) katika mji wa Marjani, kitakua na vyumba (98) vya wagonjwa pamoja na vyumba vingine (20) vya madaktari na wauguzi, baada ya kumaliza hatua ya kwanza ya kuandaa kiwanja mafundi wamekamilisha pia mchoro wa jengo”.

Akaongeza kuwa: “Aidha wamemaliza kumwaga changarawe (BRC) kwa ajiki ya maandalizi ya kuweka zege, kazi ya kuweka zige itafanywa kwa kufuata vipimo maalum, pamoja na kuwa zege hilo litachanganywa kwa kutumia viwango maalum vinavyo endana na aina ya jengo linalo jengwa”.

Kumbuka kuwa kituo hiki ni moja kati ya vituo vitatu vinavyo jengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kwenye mkoa wa Bagdad na Muthanna, pia ni sehemu ya vituo vinne vilivyo jengwa kwenye mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu, hospitali kuu ya Hindiyya katika mkoa wa Karbala na kituo cha nne kilijengwa kwa ufadhili wa hospitali ya kiongozi wa waumini (a.s) katika mkoa wa Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: