Kwa kuwakilisha Iraq: Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma kimeingiza maktaba ya Raudhatu-Haidariyya na Chuo kikuu cha Bagdad kwenye ripoti mpya ya muungano wa maktaba za kimataifa

Maoni katika picha
Muungano wa kimataifa wa jumuiya na taasisi za maktaba (IFLA) kupitia Atabatu Abbasiyya tukufu, umeiingiza maktaba ya Raudhatu-Haidariyya na ile ya chuo kikuu cha Bagdad katika mpango wa (utendaji masafa) kwa kufanya nadwa na warsha kwa njia ya mtandao, zimeingizwa katika maktaba zinazofanya harakati wakati huu wa janga la Korona, kupitia muwakilishi wa Iraq na mmoja wa wajumbe tegemezi, ambaye ni kituo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo Ustadh Hasanaini Mussawi, akasema: “Jumla ya maktaba zilizo ingizwa kwenye ripoti ya muungano wa jumuiya na taasisi za maktaba (IFLA) imefika tisa, maktaba zote za jumuiya ya Al-Ameed zimeingizwa pamoja na maktaba ya chuo kikuu cha Diyala, maktaba ya chuo cha Imamu Alkaadhim (a.s), maktaba ya chuo cha Almustanswariyya, maktaba ya chuo kikuu cha Al-Iraqiyya, maktaba kuu ya chuo cha Al-Ameed, maktaba kuu cha chuo cha Nahraini, jumuiya ya maktaba na taaluma ya Iraq pamoja na maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu iliyo kuwa ya kwanza kuingizwa kwenye ripoti hizo”.

Akasema kuwa: “Kutokana na ongezeko hilo tumefanikiwa kuinua jina la Iraq kwenye mtandao huo wa kimataifa, ambao unawanachama zaidi ya (150), milango yetu ipo wazi kushirikiana na maktaba yeyote binafsi au ya umma, maadam imekamilisha masharti na inapenda kuingizwa kwenye orodha hii ambayo hutoa ripoti za maktaba wanachama na kuzisambaza bure”.

Tambua kuwa muungano wa jumuiya na taasisi za maktaba (IFLA) tangu kuripotiwa kwa virusi vya Korona umekuwa ukiangalia utendaji wa maktaba zake wakati huu wa kipindi cha janga la Korona ambalo limeathiri kwa kiasi kikubwa utendaji wa maktaba, na wameandaa ripoti kamili kupitia maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya, ukizingatia kuwa ndio muwakilishi rasmi wa maktaba za Iraq kwenye muungano huo, pamoja na kazi nzuri ambayo wamefanya katika kipindi hiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: