Kubaini aina ya saratani kwenye maabara ya Alkafeel kwa muda usiozidi dakika (15)

Maoni katika picha
Maabara ya hospitali ya Alkafeel inamiliki vifaa tiba vya kisasa vya saratani vyenye uwezo wa kutoa majibu halisi kwa muda mfupi.

Kiongozi wa idara hiyo Dokta Nizaar Jabbaar amesema kuwa: “Idara ya maabara ilianza kazi tangu siku ya kwanza ya kufunguliwa kwa hospitali, imekuwa ikiboreshwa siku zoto, inamadaktari mahiri na vifaa tiba vyenye ubora mkubwa”.

Akaongeza kuwa: “Maabara yetu inatofautiana na zingine inamiliki kipimo chenye uwezo wa kutoa majibu ndani ya muda wa dakika (15 hadi 20)”.

Akafafanua kuwa: “Kifaa hicho kinauwezo wa kubaini aina ya saratani kama ni mbaya au nzuri, majibu ambayo yatamsaidia daktari wa upasuaji katika kuchagua aina ya upasuaji”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel imekuwa ikijitahidi kutoa huduma bora, kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa inavyo miliki na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa maradhi tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa wa aina zoto ambao wapo katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: