Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi katika mji wa Misaan wanagawa vifaa kinga na barakoa kwa watumishi wa vituo vya afya

Maoni katika picha
Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) katika mkoa wa Misaan, wamegawa vifaa kinga na barakoa kwa watumishi wa vituo vya afya hapa mkoani, kama sehemu ya kuwasaidia kupambana na janga la Korona.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: Kituo cha kwanza cha ugawaji huo ilikuwa ni hospitali ya Azal katika wilaya ya Majarrul-Kabiir, kwa kuwasiliana na muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu wa eneo hilo Sayyid Hashim Sharíy na mkuu wa hospitali Dokta Abdurazaaq Fartusi, tumegawa vifaa kinga (100) na barakoa (200).

Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu na mkuu wa hospitali hiyo wamekishukuru kikosi cha Abbasi kwa kazi kubwa kinayo fanya ya kupambana na janga la Korona.

Tambua kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimeweka kambi katika msikiti wa Koroshat kwa ajili ya kutengeneza vifaa kinga na barakoa halafu kinazigawa bure.

Kumbuka kuwa kikosi kiliunda kamati maalum ya kupambana na janga la Korona ambayo inafanya kazi ya kupuliza dawa kwenye maeneo ya makazi ya watu ndani na nje ya mkoa wa Karbala, na kinafanya kila kiwezalo kupambana na janga hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: