Kwa mara ya kwanza hapa Iraq: imetolewa nakala ya kielektronik ya msahafu uliochapishwa na Atabatu Abbasiyya kwa umakini na ubainifu mkubwa

Maoni katika picha
Kituo cha maarifa ya Quráni tukufu kuifasiri na kuichapisha chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa nakala ya msahafu uliochapishwa na Atabatu Abbasiyya ya kielektronik yenye ubora wa hali ya juu, imezidi nakala mashuhuri ya Madina kwa vitu vingi, kwanza inakubali kuchapishwa, kwa ajili ya kuifanya chapa hii inayo hitajiwa na watu wengi kuwa na manufaa zaidi.

Mkuu wa kituo cha maarifa ya Quráni tukufu, kuifasiri na kuichapisha Shekh Dhiyaau-Dini Zubaidi amesema kuwa: “Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanajitahidi kufanya kazi tukufu za kibinaadamu na kiislamu sambamba na kukitumikia kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, siku za nyuma walifanikiwa kuchapisha msahafu wa kwanza hapa Iraq chini ya uandishi wa raia wa Iraq katika kiwanda cha uchapishaji Darul-Kafeel”.

Akaongeza kuwa: “Hivi sasa wametoa nakala ya msahafu ya kielektronik yenye ubora mkubwa, miongoni mwa sifa za nakala hiyo ni:

  • - Ubainifu na muonekano mzuri, ni rahisi kusoma na kukopi au kuchapisha.
  • - Unaweza kuongeza ukubwa wa herufi kwa kiwango chochote unacho taka bila kuharibu mpangilio wake.
  • - Unapo chapisha hauwezi kufuta au kuongeza herufi au haraka katika neno lolote, kuilinda isitiwe makosa wakati wa uchapishaji.
  • - Tumetenganisha wau unganishi (wau-atfu) na neno la baada yake, unaweza kuichapisha peke yake.
  • - Tumetenganisha herufi unganishi ambazo huwekwa mwishoni mwa maneno, ili iwe rahisi kwa msomaji na mtu anayetaka kuchapisha kuunganisha aya au sura bila kukosea.
  • - Nakala hii inaujazo mdogo na rahisi kuipakua kwenye kompyuta kwa muda mfupi katika hatua ya kwanza”.

Kuhusu namna ya matumizi ya nakala hii, amefafanua kuwa: “Baada ya kufungua faili unatakiwa kuchagua (FONTS) zilizopo, kwa kubonyeza upande wa kulia wa kipanya (kiashiria), baada ya kuchagua (FONTS) faili la (Word) litafunguka na utaona neno limeandikwa (INSTALL), bonyeza neno hilo na hapo aya zote za Quráni tukufu zitadhihiri mbele yake (ALQURAN)”.

Kwa maelezo zaidi au kupakua nakala hiyo fungua link ifuatayo:

https://alkafeel.net/quran/res/rar/quranDOC.rar
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: