Jopo la madaktari katika hospitali ya Alkafeel limefanikiwa kutibu mgonjwa aliyeshindikana kupona kwenye hospitali zingine

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa upasuaji katika hospitali ya Alkafeel limefanikiwa kumtibu mgonjwa aliyeshindikana kwenye hospitali nyingi. Daktari wa upasuaji bwana Muntaswiru Difaai amesema kuwa: “Jopo la madaktari chini ya usimamizi wetu limefanikiwa kumtibu kijana mwenye umri wa miaka thelathini kutoka mkoa wa Diyala, aliyekua muathirika wa tukio la kigaidi”.

Akaongeza kuwa: “Alikuwa na hali mbaya sana, matumaini ya kupona baada ya kufanyiwa upasuaji yalikua asilimia %60”.

Akafafanua kuwa: “Alipokelewa katika hospitali ya rufaa Alkafeel, na kufanyiwa upasuaji uliochukua saa nne, tulifanikiwa kumaliza tatizo kabisa na mgonjwa anaendelea kuimarika akiwa na afya nzuri”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel imekuwa ikijitahidi kutoa huduma bora wakati wote kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa chini ya madaktari bingwa wenye uzowefu mkubwa wa kitaifa na kimataifa, jambo ambalo limeifanya kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel, hualika madaktari bingwa wa maradhi tofauti kila wakati, sambamba na kupokea wagonjwa wa aina zote waliopo katika hatua mbalimbali za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: