Hivi punde.. Ofisi ya Ayatullahi Sayyid Sistani imetangaza kuwa: Jumatano ya kesho ni mwezi mosi Dhulhijjah

Maoni katika picha
Ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani imetagaza kuwa kesho siku ya Jumatano tarehe (22 Julai 2020) ni mwezi mosi Dhulhijja (1441h).

Hayo yapo katika tamko lililotolewa na ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani kwa mtandao wa Alkafeel, lililo sema kuwa ofisi ya Mheshimiwa imethibitisha kuandama kwa mwezi wa Dhulhijja (1441h).

Kutokana na taarifa hiyo siku ya kwanza ya sikukuu ya Idul-Adh-ha itakuwa siku ya Ijumaa mwezi (10 Dhulhijja 1441h) sawa na tarehe (31 Julai 2020m).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: