Maahadi ya turathi za Mitume imetangaza ufunguzi wa awamu mpya ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) chini ya kitengo cha elimu na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza awamu mpya ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao, masomo hayo ni ya hatua ya awali ya masomo ya juu kwa wasichana walio maliza hatua ya masomo ya utangulizi.

Mkuu wa Maahadi Shekh Hussein Turabi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Masomo yatakayo fundishwa katika hatua hii ni:

  • a- Fiqhi (Sheria za kiislamu jz1/ kimeandikwa na Mhakiki Hilliy).
  • b- Usulu-Fiqhi (Halaqa ya kwanza/ kimeandikwa na Sayyid Shahidi Muhammad Baaqir Swadri).
  • c- Balagha (Tahdhibul-Balagha/ kimeandikwa na dokta AbdulHaadi Fadhili).
  • d- Nadhariyyatul-Maárifah (Madhkal ila Nadhariyyatul-Maárifah/ kimeandikwa na Shekh Ghulamu Ridhwa Fayyaadh).
  • e- Elimu ya Swarafu (Mukhtaswaru-Swarfu/ kimeandikwa na Dokta Abdulhadi Fadhili).
  • f- Nahau (Mlango wa nne katika kitabu cha Mughni Labibu/ kimeandikwa na ibun Hisham Answari)”.

Akaongeza kuwa: “Muda wa masomo katika hatua hii ni mwaka mmoja, baada ya mwaka kutakuwa na mtihadi kiwango cha ufaulu ni alama %60, aidha wanafunzi watatakiwa kuandika ripoti ya masomo, kwa sababu hatua hii inalenga kumuandaa mwanafunzi na hatua ya masomo ya juu, na kuwafundisha namna ya kujitegemea, hatua hiyo haina usomaji wa chini ya usimamizi wa mwalimu, mwanafunzi anatakiwa ajitegemee yeye mwenyewe pamoja na kazi za makundi”.

Akaendelea kusema: “Baada ya kumaliza hatua ya awali ya masomo ya juu (sutuuhu) tutaanza rasmi hatua ya masomo ya juu (sutuuhu) ambapo somo kuu litakuwa ni Fiqhi (Lumá-Demeshqiyya na Makaasibu) na katika Usulu-Fiqhi watafundishwa kitabu cha (Halaqaatul-Usuulu wa Kifayatul-Usuulu), hatua hii itakuwa na viwango tofauti, tutaeleza zaidi siku zijazo”.

Akasema: “Hatuna kizuwizi cha kupokea wanafunzi kutoka nje ya Maahadi kwa wale ambao wanapenda kujiunga na masomo haya, lakini chini ya utaratibu ufuatao:

Kwanza: atupatie faili lenye vitu vifuatavyo:

  • a- Kopi ya kitambulisho cha taifa.
  • b- Barua ya utambulisho kutoka kwa muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu wa mji anaoishi.
  • c- Cheti cha kuhitimu masomo ya sekondari (upili) au kinacho fanana na hicho.

Pili: barua ya utambulisho kutoka shule aliyosoma, pamoja na taarifa ya maendeleo yake katika masomo aliyo fundishwa kwenye hatua ya masomo ya utangulizi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: