Makumi ya vifurushi vya chakula yametolewa na mawakibu za mkoa wa Misani kwa familia za mafakiri na wahanga

Maoni katika picha
Mawakibu za Husseiniyya katika wilaya ya Musharrah mkowani Misani, zimetoa makumi ya vifurushi vya chakula kwa familia za mafakiri na wahanga ma maambukizi ya virusi vya Korona, sambamba na kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi, kupitia opresheni kubwa iliyo andaliwa na mawakibi za wilaya hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa mawakibu hizo bwana Ahmadi Wahidi Kadhim Alkhuzai amesema kuwa: “Opresheni hii ni sehemu ya opresheni nyingi zilizo fanywa na mawakibu hizo tangu lilipotokea janga la maambukizi ya virusi vya Korona, aidha ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu aliye himiza umuhimu wa kusaidia familia hizo katika mazingira haya, tumeandaa ratiba kamili ya kutoa misaada hiyo na mawakibu nyingi za wilaya hii zimeshiriki”.

Akabainisha kuwa: “Opresheni hii imeshuhudia ugawaji wa vifurushi vwenye aina tofauti za vyakula, vikiwa na chakula kibichi pamoja na kilicho pikwa, kuna mchele, mboga za majani na nyama, chakula hicho kinasaidia japo kidogo kupunguza ugumu wa maisha ya familia hizo”.

Akamalizia kwa kusema: “Hakika misaada tunayotoa ni kidogo sana ukilinganisha na mahitaji pamoja na utukufu wa familia hizo, tunamuomba Mwenyezi Mungu atupokelee hiki kidogo tunacho toa na atuondolee balaa hili katika taifa letu”.

Kumbuka kuwa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kilitangaza opresheni kubwa ya kusaidia familia za mafakiri na wahanga wa marufuku ya kutembea kama sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: