Kuanza kwa mashindano ya uhadhiri ya mwaka wa tano

Maoni katika picha
Asubuhi ya Jumatano mwezi (8 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (29 Julai 2020m) shindano la uhadhiri la mwaka wa tano limeanza, linasimamiwa na idara ya uhusiano wa vyuo na shule chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, shindano hili na maalum kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari, chini ya kauli mbiu isemayo: (kwa vidole vya jeshi letu leupe na uwajibikaji wetu taifa linapata amani).

Kiongozi wa idara ya harakati za shule chini ya idara tajwa Ustadh Mahmudu Twahir Habibu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mashindano haya yatafanyika kwa muda wa siku mbili, yamepata washiriki kutoka mikoa tofauti, hufanywa kila mwaka, mwaka huu tunafanya kwa njia ya mtandao kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa ya maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akaongeza kuwa: “Mihadhara iliyo tufikia tayali tumeiwakilisha kwenye kamati ya majaji inayo undwa na wajumbe kutoka kwenye kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, majina ya washindi yatatangazwa usiku wa sikukuu ya Idul-Adh-ha kupitia mtandao wa kimataifa Alkafeel, na kwenye ukufara wa kijana mzalende wa Alkafeel wa kwenye Facebook”.

Akafafanua kuwa: “Mashindano haya ni sehemu ya kupongeza kazi kubwa iliyo fanywa na wahudumu ya afya ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, aidha ni fursa ya kubaini vipaji vya wahadhiri”.

Kumbuka kuwa kuna zawadi kwa washindi watano wa kwanza kama ifuatavyo:

  • 1- Mshindi wa kwanza (300,000) dinari za Iraq.
  • 2- Mshindi wa pili (250,000) dinari za Iraq.
  • 3- Mshindi wa tatu (200,000) dinari za Iraq.
  • 4- Mshindi wa nne (150,000) dinari za Iraq.
  • 5- Mshindi wa tano (100,000) dinari za Iraq.

Tambua kuwa kutakuwa na vyeti vya ushiriki kwa kila atakaeshiriki mashindano hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: