Atabatu Abbasiyya tukufu inaomboleza kifo cha balozi wa Imamu Hussein Muslim bun Aqiil (a.s)

Maoni katika picha
Katika kumbukumbu ya kifo cha balozi wa Imamu Hussein na mtoto wa Ammi yake Muslim bun Aqiil (a.s), uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa utawala chini ya taratibu zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona na kuhudhuriwa na watumishi wachache wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Majlisi imefunguliwa kwa Quráni tukufu halafu akapanda kwenye mimbari Shekhe Ali Mujaan kutoka kitengo cha Dini, akaeleza utukufu wa Muslim bun Aqiil na nafasi yake mbele ya Imamu Hussein (a.s), na kwa nini bwana wa Mashahidi alimteuwa kuwa balozi wake, aidha amezungumza kuhusu namna alivyo uwawa na watawala waovu wa Umawiyya.

Majlisi hii ya kuomboleza ni muendelezo wa majlisi za misiba ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wafuasi wao watukufu, kutokana na misiba hiyo kuchukua nafasi kubwa katika nyoyo za waumini na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Kumbuka kuwa siku ya mwezi (9) Dhulhijjah ndio siku aliyo uwawa balozi wa harakati ya Husseiniyya na shahidi wa kwanza wa harakati hiyo Muslim bun Aqiil (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: