Marjaa Dini mkuu: lazima kufuata maelekezo ya afya yaliyo tolewa na mamlaka husika katika kufanya majlisi Husseiniyya za umma.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amehimiza ulazima wa kufuata maelekezo yanayo tolewa na idara ya afya wakati wa kufanya majlisi za Husseiniyya, watu wakae kwa umbali unaotakiwa pamoja na kuvaa barakoa na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Maelezo hayo yapo katika jibu lililo tolewa na ofisi ya Marjaa Dini mkuu siku ya Alkhamisi mwezi (9 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (30 Julai 2020m), lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Kufanya majlisi za nyumbani kwa muda mfupi usiku au mchana, na kuhudhuriwa na wanafamilia na watu wa karibu yao, na kusikiliza mihadhara kwenye luninga au kwenye mitandao ya intanet, majlisi za kuhusisha watu wengi lazima zifuate taratibu za afya zilizo wekwa na idara husika, watu wakae kwa umbali unao takiwa na wavae barakoa sambamba na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, pamoja na kuhudhuriwa na watu wachache kulingana na sehemu inapo fanyika majlisi hiyo kama ni sehemu ya wazi au ndani, pamoja na kutofautiana kwa mazingra ya nchi kuhusu maambukizi ya virusi vya Korona).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: