Marjaa Dini mkuu: vituo na taasisi za Dini zinatakiwa kuwasiliana na wahadhiri na kurekodi mihadhara yao kisha kuirusha mubashara kwenye luninga na mitandao ya intanet

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza umuhimu wa kuruha mubashara majlisi za Husseiniyya kwenye luninga na mitandao ya intanet, amehimiza vituo na taasisi za Dini ziwasiliane na wahadhiri wazuri na kurekodi mihadhara yao, pamoja na kuwahimiza watu wafuatilie mihadhara hiyo wakiwa majumbani kwao.

Maelezo hayo yapo katika jibu lililotolewa na ofisi ya Marjaa Dini mkuu siku ya Alkhamisi mwezi (9 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (30 Julai 2020m), lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Kurusha matangazo mubashara ya kuomboleza kwenye luninga na mitandao ya intanet, vituo na taasisi za Dini ziwasiliane na wahadhiri wazuri pamoja na waimbaji wa kaswida za kuomboleza kwa ajili ya kuwarekodi na kuwarusha kwenye luninga na mitandao ya intanet, na watu wahimizwe kufuatilia mihadhara hiyo wakiwa majumbani kwao).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: