Maahadi ya Quráni tukufu inaendelea kufundisha semina za majira ya kiangazi kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia matawi yake yote yaliyopo mikoani inaendelea kutoa semina za Quráni za majira ya kiangazi kwa njia ya mtandao, zikiwa na washiriki kutoka ndani na nje ya Iraq, wenye umri kati ya miaka (6 – 15).

Mkuu wa Maahadi ya Quráni Shekh Jawadi Nasrawi amesema kuwa: “Kama mnavyo jua Maahadi imekuwa ikifanya semina za Quráni katika majira ya kiangazi kila mwaka, mwaka huu umekua tofauti kwa sababu ya janga la Korona, kwa hiyo tunafanya semina kwa njia ya mtandao, tunafundisha masomo tofauti ya Quráni, Fiqhi, Aqida, Akhlaqi na Sira”.

Akaongeza kuwa: Wanafunzi wengi wameshiriki kwenye semina hii, kutoka ndani na nje ya Iraq, kiongozi wa kituo cha habari cha Maahadi Mustwafa Daámi amesema kuwa: “Maahadi imefanya mambo mawili ya msingi kwenye mradi huu, kuandaa masomo na kuyaweka kwenye utaratibu mzuri, na jambo la pili lilikuwa ni kuwasilisha masomo kwa wanafunzi kila siku, kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii iliyo chini ya Maahadi, pamoja na kuendelea kupokea wanafunzi wapya wanao omba kujiunga na masomo”.

Kumbuka kuwa mradi wa semina za majira ya kiangazi ni miongoni mwa miradi muhimu sana katika Maahadi ya Quráni, uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya unaupa kipaombele zaidi na kuuweka mbele katika harakati zake, kutokana na malezi mazuri yanayo patikana kwenye mradi huo.

Unaweza kufuatilia masomo kupitia mtandao wa youtube kwa link ifuatayo: http://www.youtube.com/c/HolyQuranInstitute

Au ukurasa wa facebook: https://www.facebook.com/Q.K.U.ImamAbbas

Au mtandao wa telegram: https://t.me/Online_Quran_courses.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: