Katika kuboresha asekta ya kilimo: Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kufanya mradi wa kilimo mkakati

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuanza kwa mradi mkubwa wa kilimo mkakati cha mazao tofauti, kama vile ngano, shairi, viazi mbatata na tende katika hatua ya kwanza, mazao yatakayo tosheleza mahitaji ya chakula kwa wananchi wa Iraq, pamoja na kuchangia kurudisha sifa ya kilimo katika taifa letu, mradi huu unabadilisha jangwa la Karbalaa kuwa kijani kibichi kwa kutumia maji ya visima, sehemu ya jangwa la barabara ya Karbala na Ainu-Tamru ndio unapotekelezwa mradi huu kwa kutumia mitambo ya kisasa.

Mtandao wa Alkafeel umekutana na Mhandisi Aadil Maliki ambae amesema kuwa: “Mradi huu utaingizwa katika miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu inayolenga:

  • - Kupambana na jangwa kwa kulibadilisha kuwa kijani kibichi.
  • - Kuboresha sekta ya kilimo na kuimarisha uwezo wa kujitegemea kwenye upande wa chakula.
  • - Kuweka mkoa katika mazingira mazuri.
  • - Kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira.
  • - Kuingiza mazao bora ya chakula kwenye soko la Iraq, bila kutegemea mazao kutoka nje ya nchi, na kurejesha sifa ya kilimo katika taifa.
  • - Kupunguza utegemeaji wa sekta ya mafuta.
  • - Kutoa elimu kwa wakulima kuhusu utumiaji bora wa maji kwa kutumia njia za kisasa.

Mkuu wa mradi huo Mhandisi Haidari Muhammad Shahidi Dahani amesema kuwa: “Tumeanza hatua ya kwanza ya mradi kwa kuchimba visima vitakavyo tumika kumwagilia mazao, tayali tumechimba visima (11) vinatosha kumwagilia awamu ya kwanza ya mradi, pamoja na kazi ya kuandaa ardhi kwa ajili ya kilimo”.

Akaendelea kusema: “Kila kisima kimeunganishwa na panel ya umeme wa jua yenye ukubwa wa (112) kwa ajili ya kuendesha mashine ya kuvuta maji”.

Akafafanua kuwa: “Tumepanda miche (1200) ya mitende bora ya kiiraq na tumeanza kutengeneza mkanda wa kijani unaozunguka mradi, pamoja na kuendelea kutengeneza mfumo wa kumwagilia kwa njia ya matone katika eneo lililolimwa chini ya mkakati maalum”.

Akasema: “Mradi huu umesanifiwa na kupangiliwa kisasa sawa na miradi mingine mikubwa kama huu, kazi inaendelea kama ilivyo pangwa na inatarajiwa kuisha ndani ya muda ulio pangwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: