Maktaba ya wanawake imefanya warsha kwa njia ya mtandao kuhusu umuhimu wa malezi ya familia na jamii

Maoni katika picha
Maktaba ya wanawake chini ya kitengo cha elimu na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya warsha kwa njia ya mtandao yenye anuani isemayo: (Umuhimu wa utamaduni katika familia na jamii), chini ya ukufunzi wa mtaalamu wa maendeleo ya binaadamu Ustadhat Muntaha Muhsin Muhammad.

Amezungumza kuhusu umuhimu wa maendeleo ya binaadamu katika maisha ya kila siku, na nafasi yake katika fikra na maendeleo, na ubora wa kujiendeleza binafsi kwa kufanyia kazi fikra za watu waliofaulu.

Tambua kuwa maktaba ya wanawake hufanya semina na nadwa nyingi kuhusu utamaduni, na walengwa wake wakuu ni wanawake, hualika wasomi na watafiti mbalimbali ambao huwasilisha utafiti wao na kutoa nafasi ya kujadili mambo mbalimbali ya kijamii.

Kumbuka kuwa idara ya maktaba ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaenda sambamba na maendeleo ya dunia kielimu, inaendesha miradi mikubwa ya elimu inayo saidia kuelekeza mafundisho ya Dini na taifa kwa ajili ya kulinda utamaduni, pamoja na kukuza uhusiano kati ya idara ya maktaba ya wanawake na vyuo vikuu na taasisi za dini na kisekula.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: