Madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel wamefaulu kupandikiza mfupa wa juu na chini ya mdomo kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka (18)

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanikiwa kutibu mgonjwa mwenye tatizo la kukosa meno tangu kuzaliwa kwake, kwa kumfanyia upasuaji wa aina yake.

Bingwa wa upasuaji wa uso Dokta Muammar A’raji amesema kuwa: “Jopo la madaktari chini ya usimamizi wetu wamefanikiwa kufanya upasuaji na kupandikiza mfupa pamoja na meno ya juu na chini (PRF) kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka (18)”.

Akafafanua kuwa: “Mgonjwa anaendelea vizuri baada ya upasuaji huo”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel imekuwa ikitoa huduma bora kwa vifaa vya kisasa wakati wote, kwani inamiliki vifaa tiba bora na vya kisasa zaidi, pamoja na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeifanya itoe ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa maradi mbalimbali kila baada ya muda fulani sambamba na kupokea wagonjwa wa aina zote walio kwenye hali tofauti za maradi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: