Atabatu Abbasiyya tukufu imepambwa kwa ajili ya furaha ya kumbukumbu ya Idul-Ghadiir

Maoni katika picha
Shangwe na furaha imetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa sababu ya kumbukumbu ya Idul-Ghadiir, kuta zimepambwa kwa vitambaa vilivyo andikwa maneno ya kuonyesha mapenzi na utiifu kwa kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), kuonyesha furaha kubwa iliyojaa katika nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika kumbukumbu ya kutangazwa kwake kuwa kiongozi wa waumini na khalifa wa Mtume (s.a.w.w).

Mwezi kumi na nane Dhulhijjah mwaka wa kumi hijiriyyah Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) alitangazwa kuwa kiongozi wa waumini, siku hiyo inasadifu Jumamosi ijayo mwezi (18 Dhulhijjah 1441h) ndio kumbukumbu ya tukio hilo takatifu.

Kutokana na muongozo wa idara ya afya hapa Karbala na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, Atabatu Abbasiyya tukufu haitafanya tukio lolote kuadhimisha siku hiyo, kufuatia hali ya mazingira ya afya ambayo taifa linapitia kwa sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: