Ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani imetoa tamko kuhusu tukio la kuhuzunisha la mlipuko wa Bairut nchini Lebanon

Maoni katika picha
Ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Ali Sistani imetoa tamko kuhusu mlipuko uliotokea katika mji wa Bairut, inawapa pole wananchi wa Lebanon kwa msiba huu mkubwa.

Ifuatayo ni nakala ya tamko hilo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu kwa majonzi na masikitiko makubwa kufuatia mlipuko ulio tokea katika mji wa Bairut na kusabisha vifo vya watu na majeruhi wengi, pamoja na uharibufu mkubwa wa majengo na mali, tukio ambalo halijawahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.

Tunatoa pole sana kwa wananchi wa Lebanon, hususan wahanga wa tukio hilo, tunamuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu, subira na mshikamano wakati huu mgumu, tunawaomba waumini watukufu na kila mpenda kheri duniani ashikamane na wahanga hao na kuwapa misaada wakati huu mgumu ili kupunguza athari za mlipuko huo.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu watu waliopoteza maisha na azipe subira familia zao, awaponye haraka majeruhi hakika yeye ni mwingi wa rehema mwenye kurehemu.



16 Dhulhijjah 1441h

Ofisi ya Sayyid Sistani – Najafu Ashrafu
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: