Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel ikotayali kupokea watu waliojeruhiwa katika mlipuko wa Bairut

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya Adhuhuri ya Alkhamisi (16 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (6 Agosti 2020m) umetangaza kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel ikotayali kupokea watu waliojeruhiwa katika mlipuko uliotokea nchini Lebanon na kutikisa mji mkuu wa Bairut siku ya Jumanne, kama sehemu ya kufanyia kazi tamko la Marjaa Dini mkuu alilotoa asubuhi ya siku ya tukio la kusimama pamoja na wananchi watukufu wa lebanoni, na kuwasaidia kwa kila njia itakayo wezekana kupunguza athari za mlipuko huo mkubwa.

Akasisitiza kuwa: “Hospitali ikotayali kusaidia kwa uwezo wake wote majeruhi wote watakaofikishwa kwenye hospitali hiyo chini ya kanuni za mataifa mawili”.

Akabainisha kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa tamko hilo kuonyesha kushikamana kwake na raia wa Lebanon na kusimama pamoja nao katika janga hili lililoacha mamia ya majeruhi”.

Tambua kuwa ofisi ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani ilitoa tamko asubuhi ya Jumatano na kutuma salam za rambirambi na kuwapa pole wananchi wa Lebanon kufuatia mlipuko huo, na imetoa wito kwa waumini na wapenzi wa kheri duniani washikamane pamoja nao katika kipindi hiki kigumu, na kutoa msaada kwa namna yeyote iwezekanayo, ili kupunguza athari za janga hilo.

Kumbuka kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Atabatu Abbasiyya, imesha wahi kufanya hivyo siku za nyumba, kama vile kutibu mazuwaru wa kiiraq walio jeruhiwa Sirya, kutibu waandamanaji pamoja na majeruhi wa Hashdu Shaábi na wanajeshi wa serikali, sambamba na kugharamia mamia ya wagonjwa wengine.

Tambua kuwa mji mkuu wa Lebanon Bairut jioni ya Jumanne ulitokea mlipuko mkubwa kwenye bandandari yake, uliosababisha vifo vya watu wengi na majeruhi zaidi ya (4000) na bado idadi inaendelea kuongezeka, pamoja na hasara kubwa ya mali na watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: