Madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanikiwa kumtibu mgonjwa mwenye umri wa miaka ishirini aliyekuwa na tatizo la mfupa wa kwenye pingili ya mkono

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kumtibu kijana mwenye umri wa miaka ishirini aliyekuwa na tatizo la mfupa wa mkono wa kulia.

Dakrari bingwa wa upasuaji na mifupa katika hospitali hiyo dokta Haidari Hashim amesema kuwa: “Jopo la madaktari limefanikiwa kuunganisha mfupa wa sehemu ya juu ya mkono wa kulia wa mgonjwa mwenye umri wa miaka ishirini”.

Akaongeza kuwa: “Mgonjwa alivunjika mfupa wa mkono wa kulia katika ajali ya gari”.

Akabainisha kuwa: “Vifaa tiba ilivyonavyo hospitali katika chumba cha ubasuaji ndio vilivyo tuwezesha kufanya upasuaji huo”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa matibabu bora daima kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa maradhi mbalimbali kila baada ya muda fulani sambamba na kupokea wagonjwa wa aina zote walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: