Kwa ushiriki wa watu (388) kutoka ndani na nje ya Iraq: Matokeo ya shindano la (Mnara wa Dini) yatangazwa

Maoni katika picha
Idara ya Quráni chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini kwa wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza majina ya washindi wa shindano la (Mnara wa Dini), lililofanywa kwa njia ya mtandao kusherehekea Idul-Ghadiir na kulipa jina la (Shindano la Mnara wa Dini), lililokuwa na washiriki 388 kutoka ndani na nje ya Iraq.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “shindano hili ni kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idul-Ghadiir na kuenzi utamaduni wa Quráni na Aqida, ili kufanya tukio la Ghadiir kuwa hai katika jamii yetu na kuendelea kuadhimishwa kila mwaka, kwa sababu ni miongoni mwa misingi ya Dini na kudumisha utume wa mbora wa mitume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w)”.

Akaongeza kuwa: “Mazingira ya shindano hili yalitegemea uwezo wa akili ya mshindani katika kuchambua habari zinazo elezea tukio hilo”.

Kuona majina ya waliofaulu fungua link ifuatayo: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=139283077824359&id=100630901689577&sfnsn=mo
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: