Kwa upasuaji wa aina yake.. madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanikiwa kumtibu mtu mwenye miaka zaidi ya sabini aliyekua na tatizo la saratani kwenye taya ya chini

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel mjini Karbala, limefanikiwa kumtibu bibi mwenye umri wa miaka zaidi ya sabini aliyekuwa na tatizo la saratani kwenye taya ya chini.

Dadtari bingwa wa upasuaji wa uso katika hospitali hiyo Dokta Ridhwani Twaiy amesema: “Jopo la madaktari chini ya usimamizi wetu limefanikiwa kuondoa chembechembe za saratani kwenye taya ya chini kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka (75)”.

Akaongeza kuwa: “Wakati wa upasuaji huo tumerudisha utendaji kazi wa sehemu hiyo kwa kutumia kifaa tiba cha madini”.

Akabainisha kuwa: “Hospitali inamadaktari bingwa na wauguzi mahiri wenye mchango mkubwa katika mafanikio haya, sambamba na kuwa na vifaa tiba bora na vya kisasa kwenye chumba cha upasuaji, vilivyo wezesha upasuaji huu adimu”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel siku zote hujitahidi kutoa huduma bora kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa, chini ya madaktari mahiri kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeifanya kutoa ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa wa aina zoto ambao wapo katika hali mbalimbali za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: